Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini limependekeza kuwepo kwa mifuko miwili
ya hifadhi za jamii ili kupunguza gharama kubwa ya kuiendesha na kwamba gharama
hizo ziingizwe kwenye mafao ya wastaafu.
Hayo
yalielezwa juzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Nicholas Mgaya wakati
akifungua semina juu ya elimu ya Mifuko ya Hifadhi iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Usimamizi na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
“Tanzania
inaonyesha ndio yenye mifuko mingi ya hifadhi za jamii ukilinganisha na nchi
jirani za Kenya, Uganda na Zambia ambapo imekuwa ikitumia gharama kubwa katika
kuiendesha, bora fedha hizo za uendeshaji zielekezwe katika kuboresha mafao ya
wastaafu,” alisema.
Alisema
ombi la Shirikisho la Wafanyakazi kwa Mamlaka ya SSRA na Serikali ni kuwepo kwa
mifuko miwili ya hifadhi za jamii ambapo mmoja utahusisha sekta binafsi na
mwingine watumishi wa umma ili kupunguza gharama za kuendesha mifuko hiyo.
Alisema
imefika wakati sasa washirikiane na SSRA ili waone ni namna gani wanaweza
kufanya mabadiliko hayo kwa kupandisha hesabu za ukokotoaji kwa mifuko ya
hifadhi ambayo ipo chini badala ya kushusha ile yenye kiwango cha juu.
إرسال تعليق