Mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi.BAADA ya kauli ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa klabu hiyo inamdai mamilioni ya fedha mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi kutokana na kushindwa kuitumikia timu hiyo kwa wakati mara baada ya kusajiliwa, suala hilo sasa limewekwa kiporo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema
kuwa, bado hawajaamua cha kufanya juu ya Okwi kwa kuwa wanamsubiri
mchezaji huyo amalize majukumu yake kwenye timu ya taifa ya Uganda, The
Cranes, kisha ndiyo watazungumza naye.
Okwi yupo na timu yake ya taifa kwa ajili ya mechi dhidi ya
Madagascar kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Africa (Afcon)
zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Morocco.
“Ni kweli kabisa tuna mpango wa kukutana na Okwi kwa ajili ya
kuzungumza naye lakini kwa sasa tumeliweka kiporo suala lake kutokana na
majukumu ya timu ya taifa.
“Hata hivyo jambo zuri ni kwamba baada ya mchezaji huyo kuwa huru
suala hilo tutalifanyia kazi na ni matumaini yetu tutafikia muafaka bila
ya kuwa na tatizo lolote,” alisema Njovu.
Tangu Okwi asajiliwe na Yanga ameitumikia klabu hiyo katika mechi
sita, mbili za kimataifa na nne za ligi kuu na baada ya hapo aligoma
kuendelea kuitumikia timu hiyo mpaka atakapolipwa fedha zake anazodai
ambazo ni dola 40,000 (Sh milioni 64) kiasi kilichobakia katika usajili
wake ulioighalimu Yanga dola 100,000 (Sh milioni 160).
إرسال تعليق