Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa wa Chadema, John Heche
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Kauli hiyo inatolewa ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira kusema Ukawa
wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.
Dodoma. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) nje ya Bunge umesema
hatima ya kupata Katiba Mpya utaamuliwa na wananchi na wala siyo chama
tawala.
Kauli hiyo inatolewa ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira kusema Ukawa
wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa wa Chadema, John Heche alisema hakuna nchi inayoandika Katiba kwa kushirikisha kundi moja.
Alisema Ukawa hawatarejea bungeni pamoja na vitisho vinavyotolewa na
viongozi mbalimbali wa Serikali ya CCM hadi pale mjadala wa kuijadili
Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba utakapozingatiwa.
“Acha wajidanganye kubadili kanuni, lakini mwisho wa siku wananchi
wanajua kinachofanywa na CCM, hatima ya Katiba Mpya iko mikononi mwao,’
alisema Heche na kuongeza:
“CCM haina nia ya kupata Katiba Mpya, kwani viongozi wake wamekuwa
wakisema Katiba iliyopo inafaa, jambo ambalo tunashindwa kuelewa kwa
nini imetoa mabilioni kuratibu mchakato huu.”
Katika hatua nyingine, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania
imejiunga na Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF
katika mikutano inayoendelea nchi nzima.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimbo alisema malengo mazuri ya Ukawa ndiyo yaliyowashawishi kujiunga.
Alisema taasisi zake zimeunga mkono harakati za Ukawa kutokana kwa
vile CCM imedhamiria kutupa kutupa maoni ya wananchi kupitia Rasimu ya
pili ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika Viwanja
vya Mwembetogwa mjini hapa, Katimbo alisema kilichofanywa na Wajumbe wa
Bunge la Katiba kutoka CCM ni ukiukwaji wa haki kwa wananchi.
Chanzo Mwananchi
إرسال تعليق