SPIKA wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema ni
marufuku kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya shughuli zake
ndani ya Bunge la Bajeti.
Alisema
hayo juzi bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman
Mbowe kutangaza baraza kivuli la mawaziri na kusema hicho ndiko kikosi
cha ukawa ndani ya Bunge.
Spika
Makinda alimtaka Mbowe kuhakikisha Ukawa inafanya kazi zake nje ya Bunge
na si ndani ya Bunge kwani wanapokuwa ndani ya Bunge wanakuwa ni kambi
ya upinzani bungeni na si vinginevyo.
“Ukawa
ndani ya Bunge haipo, mnakumbuka shuka kumekucha, baraza lenu ni
International Standard na miaka ya nyuma nilishawahi kuwashauri kitu
kama hicho lakini mkakidharau na kuona hakina maana, nawapongeza sana,
lakini mmekumbuka shuka kumekucha,” alisema.
Pia Spika Makinda alilitaka baraza hilo kivuli kutoa ushirikiano na wabunge wengine ili kufanya kazi ya kuendeleza watu.
“Watanzania
hawajui nani anatoka wapi ila wanachotaka ni maendeleo yatakayosaidia
kuboresha hali zao za maisha, wanataka kuona barabara nzuri na hata
mazao yao yananunuliwa,” alisema.
Uteuzi
huo ulihusisha vyama vya Chadema, CUF na NCCR Mageuzi ambapo baraza hilo
kivuli lina mawaziri 29 ambapo watashika nafasi za uongozi katika
kipindi kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
إرسال تعليق