

Fid
Q ameonekana kama anamfokea Dayna kwa kutumia mkorogo unao badilisha
ngozi yake na kuonekana mweupu kitu ambacho Fid Q amedai kuwa Dayna
anaukimbia uafrika,Mistari ya Verse hiyo iko hivi.
“Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
Soudy brown kamtafuta Fid Q ambapo alipoulizwa kuhusu hili majibu
yake alidai kuwa katika ngoma hiyo hamzungumzii Dayna Msanii bali
anamzungumzia Dayna msichana anayeishi nae kitaani maeneo ya Mikocheni
kwa Nyerere.
Dayna huyo wa kiafrika alikua mweusi sasa hivi amejichubua ngozi yake
na kuwa mweupe ambapo baadae Fid Q aliuchambua kiutaalam mstari huo na
kusema kuwa wadada wanaofanya hivyo wanaua melanie.
Ambacho ni kitu muhimu sana kwenye ngozi na hupatikana zaidi kwenye
ngozi nyeusi ya kiafrika chembechembe ambazo huilinda ngozi isiunguzwe
na jua.
Majibu ya Dayna baada ya kupigiwa simu na Soudy Brown kutaka kujua
kama ameshaisikia hiyo line ya Fid Q alichokijibu ni ameisikia na
anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa wakati huu amepunguza kidogo
kutumia mikorogo.
إرسال تعليق