Umoja Wa Watanzania Ujerumani Wazindua Tovuti

Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U) Umezindua Mtandao wake leo hii Tarehe 19.05.2011, mjini Aschaffenburg ujerumani. Mtandao huo ambao umeaza kutumika kwa lugha ya Taifa ya Ujerumani (kijerumani) upo mbioni pia kutandaza habari kwa lunga za kimataifa ikiwemo kiswahili.
 Akiongea na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti wa umoja huo mheshimiwa Mfundo Peter Mfundo amewataka wanachama wa U T U  na Watanzania wote kwa Ujumla kuwa na subira kidogo kwani mtandao huo utaanza kupatikana kwa lugha ya kiswahili kwa ajili ya kuwapasha kila taarifa na kinachoendelea kutoka kwenye umoja wenu. 

Mtandao huo  unapatikana katika www.ututz.com 
au http//www.ututz.com 
kwa mawasiliano zaidi  wasiliana na kamati.utu@googlemail.com  
kamati ya UTU inawatakia kila la heri katika kurambaza kwenye mtandao wetu.

Post a Comment

أحدث أقدم