STL ni mmoja wa wasanii waliopata bahati ya kuchaguliwa kujiunga na “Coke Studio”, kipindi kinachounganisha wasanii wakubwa kutoka kila kona ya Afrika. Baadhi yao ni Diamond Platinumz, Octopizzo, Lillian Mbabazi, Miss Karun na Waje kutoka nchini Nigeria.
Baada ya kuonekana katika msimu wa kwanza wa Coke Studio na kuiwakilisha vizuri Kenya, habari mpya ni kwamba “STL” hatakuwepo katika msimu wa pili wa Coke Studio kutokana na kutokubaliana na waandaaji wa show hiyo. Manager wa STL alisema ” waandaji wa Coke Studio wameshindwa kukubali kutulipa kiasi cha pesa tunachotaka wakisema hakiendani na bajeti waliyo nayo. Kwa hiyo tukaamua kuachana na show hiyo kwa sababu kurekodi show hiyo kunachukua mda sana”
Coke Studio ni show inayoandaliwa na Coca-Cola Company ambayo huonyesha wasanii wakubwa waimba nyimbo za wasanii mbalimbali live. Ni show ya kipekee kwani huwaunganisha wasanii wanaoimba aina tofauti tofauti za mziki na kutoka nchi mbali mbali Afrika.
Post a Comment