Miongoni mwa nyimbo ambazo zinasikika sana katika vituo vya
radio kwa sasa ni pamoja na ‘Serebuka’ ya Mwasiti Almasi, wimbo ambao
ulitoka miezi kadhaa iliyopita bila video.
Mwasiti amesema video hiyo iliyoongozwa na director Nick Dizzo imekamilika na anatarajia kuitoa wiki hii.
“Nakaribia kutoa video yangu mpya, so next week natoa video rasmi iko
tayari” Amesema Mwasiti “ni video nzuri kwakweli wataona huko kuna
wanamuziki wa bongo fleva wa kike wamefanya yao, wataona kazi nzuri ya
Nick Dizzo ndio amefanya hiyo kazi” Mwasiti ameiambia E-News ya EATV.
إرسال تعليق