Baadhi
ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini
wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa
kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini
Arusha.(Picha na Zainul Mzige).
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi
wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari
na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda
aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama
sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na
kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti
zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili
unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi
ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari
na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa
hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza
kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa
vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo
linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama
kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.
Afisa
Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari
katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la
waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.
“Kwa
sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi
mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya
habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba
ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili
kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.
Kibanda
aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna
ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari
hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha
tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa
upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka
2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina
nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa
nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.
“Kuwe
na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari
nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na
kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema
Kasongo.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse,
akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa
kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari
lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya
habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.
Mwanahabari
mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya
Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru
wa habari walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha
heshima waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila
upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale
unapokosea.
“Kuandika
habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na
kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”
Akizungumzia
suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth
Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao
na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi
katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.
Maadhimisho
hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa
MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida
mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija
ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark
Bomani.
Mwanahabari
Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia)
akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la
siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani
2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu
cha Iringa, Bw. Simon Berege.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati
wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya
Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na
wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa
kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini
Arusha.
Mwandishi
wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila
mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za
uchambuzi.
Mwanahabari
Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo
Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini
wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa
vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Mmiliki
wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid
Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa
Redio.
Makamu
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na
Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye
akichangia mada.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Picha
juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano
la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari
Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
Mwanakamati
wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
إرسال تعليق