HOMA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo
wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta
International’, wamekumbwa na ugonjwa huo, habari zimefika katika dawati
la Risasi Mchanganyiko.
Mmoja wa wanamuziki wa Twanga anayesumbuliwa na Homa ya Dengue, Bakari Kasongo ‘Mandela’.
Mtoa habari Hassan Rehani ambaye ni meneja wa bendi hiyo, alizungumza
na mwandishi wetu hivi karibuni na kuwataja wanamuziki hao kuwa ni Badi
Bakule, Ramadhan ‘Pentagoni’, Bakari Kasongo ‘Mandela’, Sabrina
Mbetembete na Natalia Mbui.
“Nimeshitushwa sana na ugonjwa huu, maana katika maisha yangu ugonjwa
ambao nilishawahi kuona unasumbua watu wa sehemu moja kwa wingi kiasi
hiki ni Kipindupindu tu, sasa hii dengue ni hatari,” alisema Rehani na
kuongeza kuwa wanamuziki hao walikuwa wamelazwa Hospitali ya
Mwananyamala na kwamba hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.
Naye mmoja wa wagonjwa hao, Rama Pentagoni, alipozungumza na
mwandishi wetu alisema anaendelea vizuri, huku akiuelezea ugonjwa huo
kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu
إرسال تعليق