
Watu watano
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Ilala, kujibu mashitaka ya
kuvunja msikiti.
Watu hao ni Mohamed Ngwai (31), Issa Karim(40), David
Kambarage (32), Melkiori Utoh (33)na Athuman Msagati (30).Wakili wa Serikali,
Ester Kyala alidai mbele ya Hakimu John Msafiri kuwa Mei 2 mwaka huu
eneo la Zanaki Wilaya ya Ilala, washitakiwa hao walivunja msikiti wa Satan Zamra.
Washitakiwa walikana mashitaka. Kati ya hao, Ngwai na
Utoh waliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Msafiri aliwataka kuwa na wadhamini wawili wa
kuaminiwa, watakaosaini kulipa Sh
milioni moja.
Wakati huo huo, mkazi wa Mwananyamala Kisiwani
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Ilala, kujibu mashitaka ya wizi wa
kutumia silaha.
Wakili wa Serikali, Hilda Kato alidai mbele ya Hakimu,
Alfred Sachore kuwa Oktoba 13 mwaka 2011
maeneo ya Kinyerezi Wilaya ya Ilala,
mshitakiwa aliiba Sh milioni 1.7, dola za Marekani 400.
Vitu vingine ni simu ya mkononi aina ya Samsung yenye
thamani ya Sh 400,000, kompyuta ndogo ya Sh 1,600,000, vyote vikiwa na thamani
ya Sh milioni 5.2, mali ya Angumwike Lameck.
Kabla ya tukio hilo, mshitakiwa alitumia kitu chenye
ncha kali, kumtishia Lameck ili kufanikisha wizi. Mshitakiwa alikana mashitaka
hayo na yaliahirishwa hadi Mei 30 mwaka huu watakapoanza kusikiliza ushahidi.
إرسال تعليق