Mahakama imeagiza watoto watatu wa marehemu Michael Jackson,
Prince, 17, Paris, 16 na Blanket , 12 kuwa wanalipwa dola milioni 8
(zaidi ya shilingi bilioni 13) kila mwaka kwaajili ya matumizi yao
mbalimbali.
Matumizi ya watoto hao wanaoishi na bibi yao Katherine Jackson na
binamu yao T.J. Jackson jijini Los Angeles, California, watapewa dola
milioni 3 kwaajii ya ada ya shule, $300,000 kwa likizo na $600,000 kwa
timu ya walinzi binafsi. Mahakama hiyo pia imeagiza watumie $200,000 za
ziada kila mwaka kupanga nyumba.
Paris, Prince na Blanket wakiwa na bibi yao
Kama haitoshi, Paris, Prince na Blanket kila mmoja atakuwa akipokea
$15,000 kwa mwezi za kutumia huku bibi yao akipewa dola milioni 1.2 kwa
mwaka kwa kuwaangalia.
Eneo la nyumba ya Michael limepanda thamani kutoka £3.5 million hadi £400 million tangu kifo chake miaka mitano iliyopita.
Post a Comment