Watoto wa Michael Jackson kupewa tshs bilioni 13 kila mwaka kwaajili ya mahitaji yao .


Mahakama imeagiza watoto watatu wa marehemu Michael Jackson, Prince, 17, Paris, 16 na Blanket , 12 kuwa wanalipwa dola milioni 8 (zaidi ya shilingi bilioni 13) kila mwaka kwaajili ya matumizi yao mbalimbali.
ku-xlarge
Matumizi ya watoto hao wanaoishi na bibi yao Katherine Jackson na binamu yao T.J. Jackson jijini Los Angeles, California, watapewa dola milioni 3 kwaajii ya ada ya shule, $300,000 kwa likizo na $600,000 kwa timu ya walinzi binafsi. Mahakama hiyo pia imeagiza watumie $200,000 za ziada kila mwaka kupanga nyumba.
article-0-0F01E17F00000578-441_634x428 Paris, Prince na Blanket wakiwa na bibi yao
Kama haitoshi, Paris, Prince na Blanket kila mmoja atakuwa akipokea $15,000 kwa mwezi za kutumia huku bibi yao akipewa dola milioni 1.2 kwa mwaka kwa kuwaangalia.
Eneo la nyumba ya Michael limepanda thamani kutoka £3.5 million hadi £400 million tangu kifo chake miaka mitano iliyopita.

Post a Comment

أحدث أقدم