Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni amelezwa toka jana katika
hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa
Dengue.
Dr Cheni akiwa hospital
Akizungumza na Bongo5 leo Dr Cheni amesema kuwa bado hali yake sio nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili kupoteza nguvu.
“Bado ni nipo hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui
unaitwa Dengue,” amesema. “Bado hali yangu sio nzuri kabisa,yaani
naumwa,napungukiwa damu,mwili unauma,kwahiyo yanai bado ninaumwa,hii
homa ilinianzia wiki iliyopita sema nilikuwa bado hawajaigundua ila jana
ndio wameingundua,” ameongeza.
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba Watanzania wamuombee kwani bado hali yake sio mzuri.
Dr Cheni akipewa huduma na msanii mwenzake wa filamu
إرسال تعليق