Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Blantyre nchini Malawi kwa
ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga aliyefarikii dunia tarehe
09 mei, 2014 Jijini na Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa tarehe 14
Mei, 2014. Mhe. Membe anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mazishi hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick Tsere akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mapokezi.
Mhe.
Membe akijaribu kumwelezea Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda namna
alivyozipokea taarifa za kifo cha Balozi Flossie. Kushoto kwa Mhe. Rais
Banda ni mume wake Jaji Mkuu Mstaafu Banda na kulia kwa Mhe. Membe ni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Ephraim Chiume.
Baadhi
ya Wananchi wa Blantyre na sehemu nyingine za Malawi wakiwa uwanjani
hapo wakati wa mapokezi ya Mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga.
Mhe. rais Banda akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule.
Mhe.
Rais Banda akisalimiana na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara
ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
إرسال تعليق