
YAYA Toure yupo nchini Qatar kupata matibabu ya ugonjwa usiofahamika kabla ya kujiunga na Ivory Coast kwenye kambi ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Marekani, shirikisho la Ivory Coast limesema jana ijumaa.
Yaya
ni mchezaji pekee anayekosekana katika kikosi cha wachezaji 28
kilichotajwa na kocha Sabri Lamouchi kwa maandalizi ya awali ya kombe la
dunia yaliyoanza alhamisi mjini Dallas.
Kiungo huyo atakwea pipa kuelekea Marekani alhamisi ijayo ili kujiunga na wenzake, shirikisho limeongeza katika taarifa yake.
Madaktari wa Hospitali ya Aspetar
Orthopaedic na Sports Medicine mjini Doha wamethibitsha kulazwa kwa
mwanasoka huyo bora wa Afrika kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "Majeruhi
ndogo`
Toure
alipata majeruhi ya mguu katikati ya aprili, lakini alirudi uwanjani
baada ya wiki mbili kuisaidia Manchester City kubeba ubingwa wa ligi kuu
soka nchini England.
Katika mchezo wa mwisho ambao Man City
waliifumua West Ham, mei 11 mwaka huu, Yaya alitolewa kipindi cha pili
kwa madai kuwa alipata majeruhi ya nyama za paja.

Mtu muhimu: Mashabiki wa Ivory Coast wana matumaini ya kuona Toure anakuwa fiti kabla ya fainali za kombe la dunia.
إرسال تعليق