YOU HEARD: WEUSI WAPINGA FID Q KUWATAMBULISHA JUKWAANI.

Jana usiku kwenye Show ya Adam Mchomvu kulitokea hali ya sintofahamu hahahaaha baada ya Member wa Kundi la Weusi kuchomoa wasipandishwe kwenye stage na Mc ambaye ni Msanii mwenzao Fid Q, hiyo ilikua ni mida ya saa kumi kumi usiku wakati ilipofika zamu Weusi kupanda kwenye stage sasa baada ya Nikki wa Pili na Joh Makini kukataa Fid Q ikabidi awaruhusu kufanya wanachotaka kwa kuwapa Mic wasanii hao wakapanda na kuperform Ngoma ya Gere,
Akizungumzia Tukio hilo Fid Q amesema haoni tatizo kwa Weusi kufanya hivyo ila yeye binafsi hana tatizo na Kundi hilo.
Nilipomtafuta msemaji wa Weusi Nikki Wa Pili akasema ni kweli walikataa Fid Q asiwapandishe kwa kuwaita ili kuongeza mzuka wanapopanda kuliko Watajwe kuwa wanapanda Shangwe litapigwa lakini wakipanda wao haitokua Surprise kwasababu Mc atakua amesha Tease, ila na wao hawana Tatizo lolote na Fid Q

Post a Comment

أحدث أقدم