37 wauawa katika wizi wa mifugo DRC

Watu wasiopungua 37 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika hujuma ambayo imetajwa kuwa ni ulipizaji kisasi kufuatia wizi wa ng'ombe. 

Tukio hilo limejiri jana Jumamosi katika kijiji kimoja mkoani Kivu Kaskazini na imearifiwa kuwa kati ya waliopoteza maisha ni mwanamke na watoto ambao walipigwa risasi na kudungwa visi au kuchomwa moto ndani ya nyumba zao. 

Baadhi pia wameuawa wakiwa ndani ya kanisa kijijini hapo walipokuwa wakikimbilia hifadhi.
Waathirika wote wa hujuma hiyo ni wa kabila la Bafuliru. 

Bado haijabainika ni nani hasa aliyetekeleza hujuma hiyo lakini kwa muda sasa kumekuwepo na mzozo baina ya watu wa kabila la Bafuliru na Warundi wanaoishi katika eneo hilo. 

Gavana wa Kivu Kusini Marcellin Cishambo amethibitisha kuwa mgogoro huo ulikuwa wa mifugo na kuongeza kuwa tatizo kubwa ni kwamba karibu kila mtu ana silaha katika eneo hilo.
Eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likikumbwa na machafuko ya mara kwa mara tokea mwaka 1998.

Post a Comment

أحدث أقدم