
Kutokana na hali hiyo, ndio maana Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) hadi sasa imeshasajili na
kuruhusu kuwepo sokoni bidhaa za vipodozi vyenye viambato vya mmea wa Aloe
Vera.
Vipodozi hivyo vilivyosajiliwa na TFDA ni 70, zikiwemo sabuni, dawa za
meno, mafuta ya kujipaka, mafuta ya kuoshea nywele na vipodozi vya kupaka
usoni.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kebwe Stephen Kebwe alisema hayo wakati akijibu swali la Waride Bakari
Jabu wa Kiembe Samaki (CCM).
Alisema hakuna tafiti
zilizofanyika duniani kuhusu matumizi ya mmea wa Aloe Vera, ila ulikuwa
ukitumika kwa matumizi mbalimbali na Wamisri wa Kale miaka 2000 iliyopita na
kuonesha manufaa makubwa katika matumizi hayo.
Akifafanua, alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia TFDA,
imefanya tathmini mbalimbali kuhusu matumizi ya mmea huo, kutumika kama
mojawapo ya kiambato salama katika bidhaa za vipodozi.
“Hii hufanyika katika kipindi cha usajili ambapo viambato vyote
vilivyoorodheshwa katika kila kipodozi hufanyiwa tathmini ya kina kuona kama
matumizi yaliyotajwa na mtengezaji ni sahihi, kwa aina ya kipodozi
anachotarajia kukiweka sokoni, ikiwemo viambato vyake” alisema.
Naibu Waziri alisema mmea wa Aloe Vera una viambato takribani 126 na
viambato hivyo vina manufaa mengi katika mwili wa binadamu, ambapo vikitumika
katika vipodozi, husaidia kulainisha, kung’arisha ngozi na kuondoa mpauko wa
ngozi na pia kuikinga na mionzi ya jua. Hutumika pia kurutubisha nywele na
kuzifanya ziwe imara na kulinda kinywa na meno inapotumika kwenye dawa za meno.
Katika swali lake, Jabu alisema “Katika miaka ya karibuni bidhaa
zinatozokana na mmea wa Aloe Vera zimezagaa katika maeneo mengi hapa nchini na
hutumika kutengenezea sabuni, mafuta ya kujipaka n.k. Je Serikali imeshafanya utafiti
kuhusu matumizi ya mmea huo?”
إرسال تعليق