Bin Slum Tyres Company Limited yaingia mkataba wa miaka miwili na Mbeya City

Kampuni ya Binslum Tyres Co. Ltd....chini ya Mkurugenzi wake, Nassor Binslum sasa imeingia mkataba wa miaka miwili wa shilingi 360 milioni na klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya.
Katika mwaka wa kwanza, Mbeya City itapokea kiasi cha shilingi 180 milioni, na mwaka wa pili itapokea kiasi kama hicho....watavaa jezi yenye nembo ya RB ikiwa ni betri maarufu za kampuni hiyo. 

Kampuni ya Bin Slum Tyre Company Limited leo imeingia mkataba rasmi wa kuidhamini timu ya soka ya Mbeya City Council ya jijini Mbeya katika hafla fupi ya utiaji saini mkataba huo uliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za jiji la Mbeya.
Mkataba huu utakuwa wa miaka miwili, ambao utawafanya Mbeya City kunufaika na kiasi hicho cha fedha kwa muda huo wote wa mkataba.
Akiongea wakati wa utiaji saini wa mkataba huo jijini Mbeya, Mkurugenzi wa , Binslum Tyre Mohamed Binslum, alisema “Tumefikia makubaliano haya baada ya kuona uongozi wa timu ya Mbeya City umejipanga vizuri katika kuendesha timu yao, na kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Jiji la Mbeya pamoja na mikoa ya Kanda ya Kusini, hivyo itakuwa ni fursa nzuri kwa kuzitangaza betri zetu za RB ambazo pia Mbeya ni soko letu kubwa”.” Kampuni yetu ina bidhaa nyingi kama vile aina nzuri ya matairi ya Double Star na Vee Rubber”. Aliongeza Binslum.

Post a Comment

Previous Post Next Post