
Gari
ambalo atakabidhiwa mshindi wa shindano kubwa nala kipekee
linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mkoa wa Tanga, Nice & Lovely
Miss Tanga 2014 tayari limepelekwa mkoani humo na sasa lipo katika
maegesho ya magari katika hotel ya Mkonge.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D
Promotion ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema
mwaka huu wampaniakuhakikisha wanapata washiriki wenye sifa na viwango
lengo likiwa ni kuhakikisha mshindi anakuja kutwaa taji la Redds Miss
Tanzania mwaka huu.
Irene amesema mwish wa kuchukua
na kurudisha fomu za kuhiriki shindano hilo ni jumampili hii ya tarehe
08 June 2014, na kambi rasmi itaanza jumatatu ya tarehe 09 June 2014
katika hotel ya Tanga Beach Resort.
Shindano la Nice & Lovely
Miss Tanga litafanyika June 21′ 2014 katika Hotel ya Mkonge. Wadamini
waliodhamini shindano hili ni Nice & Lovely, Eatv, Redds, Breeze Fm,
Tanga Beach Resort, Mwambao Fm na Rweyunga Blog
إرسال تعليق