Mkurugenzi
Mtendaji
wa Kampuni ya AP Media & Consult Ltd, Peter Keasi ametaka gazeti la Mawio
limlipe Sh bilioni mbili kama fidia, kwa kile anachodai kuchapisha habari
ambazo zimesababisha kushuka kwa hadhi yake na ya kampuni na hivyo kumwathiri
kibiashara.Anatuhumu
gazeti hilo, katika toleo la Juni 5 hadi 11 mwaka huu, kuchapisha habari hizo
chenye kichwa cha habari cha ‘CCM
kutumia bilioni 3.4 kujitangaza’.
Wakili
Kiongozi, Alloyce Komba amemwandikia mhariri wa gazeti hilo la Mawio akisema
habari iliyoandikwa, imemdhalilisha na kumkashifu mteja wao. Aidha alisema
haikuzingatia maadili ya uandishi wa habari yanayoelezwa na Kanuni za Maadili
kwa Wanahabari Tanzania za mwaka 2010 .
“Mteja
wetu ana hadhi kubwa ya kiuongozi, kitaaluma, kibiashara na kitabia pamoja na
hadhi ya kampuni yake amesikitishwa sana habari hiyo iliyomshushia hadhi kwa
kiasi kikubwa kwani habari hiyo ina taarifa zisizo sahihi, zisizo za kweli na
kutoka vyanzo visivyofahamika,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo ya wakili, pamoja na masuala mengine, habari husika
ilisema AP Media ilipewa kazi ya Sh bilioni 3.4 na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kukitangaza wakati wa kuelekea sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwake Februari
mwakani. Pia ilidai mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo ni mwandishi wa habari wa
magazeti ya serikali ya Daily News na HabariLeo.
“Kampuni
haijapewa kazi yoyote kwa zabuni au kuteuliwa peke yake kuitangaza CCM kwa Sh
bilioni 3.4…,” ilisema taarifa hiyo iliyokanusha Keasi kuwa mfanyakazi wa Daily News na HabariLeo
kwa kuambatanisha na barua ya kuacha kazi katika Kampuni ya Shirika la Magazeti
ya Serikali (TSN) miaka miwili iliyopita.
Ikinukuu
sehemu za habari hiyo, taarifa hiyo ya wakili imesema mteja wao anaonekana ni
mhujumu uchumi au ni fisadi kwa wananchi. Ilisisitiza, “mteja wetu hajawahi
kuwa mhujumu wa uchumi au kuwa fisadi tangu akiwa mfanyakazi wa shirika la
magazeti ya serikali kwa miaka 14 na kupewa hati ya utumishi mzuri .”
Kuhusu
habari ya kusahihisha, gazeti hilo limetakiwa likanushe katika ukurasa wa
kwanza wa toleo lijalo kwa kukiri makosa yaliyofanyika kimaadili na kisheria.
Post a Comment