
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production (T) Limited Bw.
Emmanuel Mahendeka wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Msanii
itakayoadhimishwa tarehe 25 Oktoba,Siku ya Msanii inaratibiwa kwa
ushirikiano baina ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA na Kampuni hii ya
Haak Neel Production. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Kaimu Katibu
Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla
ya uzinduzi wa siku ya Msanii itakayoadhimishwa tarehe 25 Oktoba, Hafla
hii imefanyika mwishoni mwa wiki hii katika Hotel ya Sea Cliff jijini
Dar es Salaam.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production (T)
Limited Bw. Emmanuel Mahendeka wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya
Msanii,mapema wikiendi hii, jijini, katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko na Kaimu Katibu wa BASATA Bw.
Godfrey Lubejo Mungereza.

Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
(katikati) akishiriki kuwakumbuka Wasanii waliotangulia mbeleza za
haki, kabla ya kuendelea na hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaanii
itakayokuwa inaadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari Bibi. Sihaba Nkinga, Mkurugenzi Mkuu wa Haak
Neel Production Bw. Emmanuel Mahendeka na Kaimu Katibu Mtendaji wa
BASATA Bw. Godfrey Mungereza.

Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akielezea kwa
ufupi histori ya Siku ya Msanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku hiyo
itakayokuwa ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.

Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Haak Neel Production (T) Ltd Bw. Emmanuel Mahendeka
akizungumza na wadau wa sanaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya
Msaanii iliyozinduliwa mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipiga
Gitaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msanii itakayokuwa
ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka

Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni wa India hapa nchini Bibi. Chitra Suresh (wapili
kutoka kulia) akifuatilia baadhi ya kazi za wasanii wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Siku ya Msanii mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Mwanamitindo
mkongwe Asiah Idarius wa kwanza akiwa na baadhi ya wanamitindo wake
wakati wa hafla ya uzinduzi wa hafla Siku ya Msanii mapema wikiendi hii.

Wasanii
wa Kikundi cha Ngoma kutoka Dodoma wakitumbuiza wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipokea
zawadi ya gauni kutoka kwa mbunifu wa mavazi na Mwanamitindo Asiah
Idarius(katikati) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema
wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (mwenye
koti jeupe) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga wakiwa
katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa wakati wa hafla uzinduzi wa
Siku ya Msanii iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Post a Comment