
KOCHA Luiz Felipe Scolari 
amesema kitendo cha mashabiki kuwazomea wachezaji wa tiimu ya Taifa ya 
Brazil katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Serbia jana ijumaa haina 
tatizo kwake na kwa wachezaji wake kwani wapo tayari kwa mazingira kama 
hayo. 
Selecao walihangaika kuvunja 
ngome imara ya Serbia katika dimba la Sao Paulo mpaka Fred alipofanikiwa
 kupenya katika dakika ya 58 na kufunga bao hilo pekee. 
Mashabiki walikosa uvumilivu na 
kujikuta wakiwazomea wachezaji wao kwa soka `mbofu mbofu` dhidi ya 
Serbia, lakini Scolari hana tatizo na kitendo hicho.
“Ni kitu cha kawaida,” Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari wa Brazil. “Ilitokea Goiania na sehemu nyingine”. 
“Haikuwa tatizo kwa mchezaji wangu yeyote. Wako tayari kwa hili”. 
“Lakini baada ya filimbi ya mwisho, asilimia 65 ya mashabiki 67,000 waliridhishwa”
Post a Comment