LAPF YAMWAGA MIKOPO KWA WANAOSOMA VYUO VIKUU

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (LAPF) umeanzisha huduma mpya ambayo itasaidia wananchama wake wenye mipango ya kupata elimu ya juu kuweza kujipatia mikopo kwa ajili ya kufanikisha adhama hiyo.
Huduma hiyo itawawezesha kujiendeleza vyuo vikuu vya hapa nchini na nje ya nchi.
Akizungumza ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji Eliudi Sanga, alisema lengo la kuanzisha utaratibu huo ni kumnufaisha mwanachama kielimu.
Pamoja na kutoa maelezo hayo aliwataka wanachama na wananchi kwa ujumla kuchangamkia mikopo hiyo ya elimu ya juu.
Aidha alisema kwamba mfuko huo utatoa huduma kwa wanachama, watumishi wa umma,wafanyabiashara na wajasirimali mbalimbali ambao wanaweka akiba zao za uzeeni katika mfuko huo.
Kwa sasa mfuko huo unatoa mikopo ya nyumba ikiwa lengo ni kuboresha maisha ya wanachama wake.
LAPF pia hutoa mikopo kwa vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa ambavyo vina wanachama wachangiaji katika mfuko huo.
Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama, Valerian Mablangeti amesema  mfuko umeweka kiwango cha chini cha riba kwa mikopo yake ikiwa ni juhudi za kuwanufaisha wanachama wake kwa kujipatia mikopo hiyo.
Mfuko huo pamoja na kutoa mikopo hiyo kiwemo ya makazi pia inatoa mafao ya uzazi. Fao hilo ni moja ya mafao sita yanayotolewa kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa LAPF, Rose Metta amesema kwamba mfuko huo umewekeza katika majengo ya biashara. Majengo hayo ni pamoja na Millennium Tower, LAPF tower na Mwanza Comercial Complex ambalo bado linajengwa kwa ushirikiano wa LAPF na jiji la Mwanza

Post a Comment

Previous Post Next Post