WAJAWAZITO 900 WAJIFUNGULIA KWA WAKUNGA WA JADI

Wajawazito wapatao 900 wamejifungilia kwa wakunga wa jadi  wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa kwa kipindi kilichoanzia Januari  hadi Mei mwaka huu.
Mganga Mkuu wa Wilaya  ya Kalambo, Dk Akilimali Mponzemenya alisema wanawake hao hao  waliojifungulia kwa wakunga wa jadi  kwa kipindi  hicho  cha miezi  takribani mitano,  ni asilimia 25  ya akina  mama 2,685  waliojifungua  katika  vituo  vya kutolea  huduma ya afya wilayani  humo.
Kwa upande wa huduma ya wagonjwa  majumbani, Dk Mponzemenya  alieleza kuwa idadi ya  wagonjwa 560 ambao wanaishi na Virusi Vya Ukimwi, wanahudumiwa majumbani na kati yao  wanaume  ni 218  na wanawake 342.
Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya Afya wilayani humo kuwa ni pamoja na baadhi ya akina mama kuendelea kujifugulia kwa wakunga wa jadi  badala  ya  kwenda  kwenye vituo  vya kutolea  huduma ya afya.
Changamoto  zingine alizitaja kuwa  ni  uhaba wa watumishi  wa afya wenye taaluma  katika  vituo vingi  vinavyotoa huduma pamoja na upungufu  wa vyombo  vya  usafiri  yakiwemo  magari na pikipiki .
Pia  kitengo  cha  dawa  wilayani  humo  hakina  stoo  ya kudumu  kwa ajili ya  kuhifadhia na hivyo dawa kutunzwa eneo lisilo rasmi.

Post a Comment

Previous Post Next Post