ZITTO KABWE ATAKA BUNGE KUDHIBITI WATENDAJI SERIKALINI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji.
Taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, kuhusu madai ya kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika akaunti ya 'Tegeta Escrow Account' na sio kulipwa katika akaunti ya PAP.
Alidai kwamba watendaji wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge.
Zitto alisema watendaji  wa aina hiyo kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo; bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na polisi ili kuchunguza na kuchukua hatua.
Alisema ipo haja ya kufumbua macho kuona na kuondoa  hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo ya kisiasa na kuwa wazalendo katika kusimamia utaifa.
Zitto alisema inatarajiwa kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa suala hilo na TAKUKURU iwafikishe mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao
serikalini.
Kadhalika alisema uchunguzi huo ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini

Post a Comment

Previous Post Next Post