
Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha
Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema
waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa
na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu
wanaohitaji msaada.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH
NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi
30.
Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa
kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za
akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.CHANZO MICHUZI BLOG
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye
hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE
amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la
mguu wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA
MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo
Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya
ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata
watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa
ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako
kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN
Post a Comment