
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Shirika la International Health
Partiners (IHP)-JEMA Tanzania, Mama Mary Ellen Kitundu mara baada ya
kuwasili katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo, mkoani Pwani. Mama Salma
alikwenda kijijini hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la hospitali
ya watoto inayojengwa na Shirika la IHP-JEMA Tanzania tarehe 10.6.2014.
Katikati ni Mkurugenzi wa Mradi huo Dkt. Jesse Kitundu.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Ndugu Ahmed Kipozi wakitembelea eneo linalojengwa hospitali ya watoto
itakayo kuwa na uwezo wa vitanda 500 katika kijiji cha Zinga huko
Bagamoyo tarehe 10.6.2014.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na wananchi
wa Kijiji cha Zinga wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la
hospitali ya watotot itakayokuwa na uwezo wa vitanda 500 tarehe
10.6.2014.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi
wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto katika Kijiji cha
Zinga huko wilayani Bagamoyo tarehe 10.6.2014. Kushoto kwa Mama Salma ni
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi.


Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda mti kwenye eneo linalojengwa
hospitali ya watoto katika kijiji cha Zinga wilayanI Bagamoyo mara baada
ya kuweka jiwe la msingi.


Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
serikali, shirika la IHP-JEMA Tanzania na viongozi wa Kijiji cha Zinga
mara baada ya sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya
watoto kijijini hapo tarehe 10.6.2014. (PICHA NA JOHN LUKUWI).
إرسال تعليق