KOCHA Msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kuwa mpaka sasa
haelewi iwapo atakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Yanga kwani Kocha
anayekuja Marcio Maximo huenda akawa na mapendekezo yake.
Mkwasa alisema: “Sijajua itakuwa vipi atakapokuja
Maximo kwa sababu, huenda akaja na mahitaji tofauti ambayo sijui kama
yatakuwa na faida kwangu au vipi.”
“Akipenda kufanya kazi na mimi sitakataa kwa
sababu naamini nitakapokuwa na yeye tutaweza kufanya vizuri zaidi, ni
kocha ambaye ana heshima yake na ninamfahamu tangu alipokuwa
akiifundisha Taifa Stars.”
- MwanaSpoti
- MwanaSpoti
Post a Comment