Mkwasa: Nikitemwa poa tu

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kuwa mpaka sasa haelewi iwapo atakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Yanga kwani Kocha anayekuja Marcio Maximo huenda akawa na mapendekezo yake.
Mkwasa alisema: “Sijajua itakuwa vipi atakapokuja Maximo kwa sababu, huenda akaja na mahitaji tofauti ambayo sijui kama yatakuwa na faida kwangu au vipi.”
“Akipenda kufanya kazi na mimi sitakataa kwa sababu naamini nitakapokuwa na yeye tutaweza kufanya vizuri zaidi, ni kocha ambaye ana heshima yake na ninamfahamu tangu alipokuwa akiifundisha Taifa Stars.”
- MwanaSpoti

Post a Comment

أحدث أقدم