MATUKIO YA SEND OFF YA MCHUMBA WA MBUNGE JOSHUA NASSARI.KESHO KUFANYA HARUSI YA ALAIKI.
 |
Askofu
Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua
Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko
wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii. |
 |
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake
Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani
kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru. |
 |
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa amekumbatiana na
Mchumba wake Bi Anande Nnko muda mfupi baada ya kumtafuta kwa muda
katika sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwa Bi Harusi Mtarajiwa
,Meru. |
 |
Bi
,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe
Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika
nyumbani kwao Meru. |
 |
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimvisha pete ,Mchumba
wake Anande Nnko akati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani
kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho
anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste,
Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya
Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika
viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa Mujibu wa Mh Nassari
,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote
wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru
Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.
"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi
sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu
la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy
grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu,
Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.
Na ssari amesema watu zaidi ya
8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo
viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .
Kwa hisani ya Busagaga's Orijino
إرسال تعليق