
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02.06.2014.
- MTU MMOJA AMEKUTWA AMEUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI.
- MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA RISASI KIFUANI KWA BUNDUKI/SILAHA.
- WATU WATANO WANASHUIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA ROBERT BUKUKU (26) MKAZI WA KIJIJI CHA IPANGA ALIKUTWA AMEUAWA KWA
KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
01.06.2014 MAJIRRA YA SAA 23:00 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LUKWEGO,
KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA KUVUNJA
NA KUIBA KATIKA KANISA LA TAG-IBOLELO. KANDO YA MWILI WA MAREHEMU
KUMEKUTWA VITU VILIVYOIBWA MALI YA KANISA HILO AMBAVYO NI PAMOJA NA
GENERATOR MOJA NDOGO AINA YA BIBLA-YAMAHA, VITI 8 VYA PLASTIKI, SAA MOJA
YA UKUTANI AINA YA SAMAY, SPANA 11 ZA AINA MBALIMBALI, MKEKA MMOJA,
MAUA MAWILI YA MEZANI NA KITAMBAA KIMOJA.
AIDHA WATUHUMIWA WATANO
WAMEKAMATWA 1. HEZRON MALIYABIBI (50) MCHUNGAJI –TAG-IBOLELO 2. KENEDY
GWALUGANO (29) MKAZI WA LUKWEGO 3. JOEL MWAKYUSA (44) MWENYEKITI
KITONGOJI CHA MASUNGWA 4. BENSON KAJUNI (48) MKAZI WA KIKOTA NA 5. KAIRO
HASSAN @ MJEGE (38) MKAZI WA LUKWEGO.
KATIKA TUKIOP LA PILI:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA FURAHA WILSON @ MATAKO (37) MKAZI WA KIJIJI CHA ICHENJEZYA ALIUAWA
KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI KWA KUTUMIA SILAHA/BUNDUKI AINA YA S/GUN
ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
01.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI KATIKA KJIJI CHA BARA KATA YA
BARA TARAFA YA ITAKA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. KANDO YA MWILI WA
MAREHEMU IMEKUTWA SILAHA BASTOLA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA INAYOTUMIA
RISASI ZA SHORT GUN IKIWA NA RISASI MOJA KWENYE MTUTU. AIDHA KWENYE
SURUALI ALIYOKUWA AMEVAA MAREHEMU IMEKUTWA RISASI MOJA YA S/GUN.
AIDHA, MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA
NA JERAHA KUBWA KIFUANI NA MGONGONI. AIDHA INADAIWA/INASEMEKANA MAREHEMU
ALIKUWA NI MHALIFU SUGU NA MZOEFU. CHANZO KINACHUNGUZWA.
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SARAH ATHUMAN (28)
MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO]
UJAZO WA LITA KUMI [10] KWENYE KAMBI YAKE YA KUCHIMBIA DHAHABU.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
01.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA KASAKALAWE, KATA
YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
AIDHA, MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA PIA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA KILO TATU [03] KWENYE KAMBI YAKE YA KUCHIMBIA DHAHABU.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA LAMECK ALINDA (55) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AKIWA NA BHANGI
UZITO WA KILO KUMI [10] IKIWA KATIKA KIKAPU KILICHOFUNGWA KWENYE
BAISKELI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
01.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:20 JIONI KATIKA KIJIJI CHA KASAKALAWE, KATA
YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
KATIKA MSAKO WA TATU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ANTHONY LUKAS
(19) NA 2. ISAKA KALUKA (24) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IHOMBE WAKIWA NA
BHANGI UZITO WA GRAM 750.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA
KATIKA KIJIJI CHA IWANGA, KATA YA IHOMBE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA
WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA/POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA KUUZA
BHANGI/POMBE HARAMU YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment