
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 02 Juni, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema wakati Serikali
imeelekeza nguvu zake katika kujenga miundombinu ya mifumo ya
tekinolojia ya habari na mawasiliano nchini changamoto kubwa ni
kuielimisha jamii kuamini kuwa matumizi ya tekinolojia hiyo kuwa ni
muhimu katika kufanikisha shughuli zao za maisha ya kila siku.
Akizungumza na Makamu wa Rais Mwandamizi wa
Kampuni ya ZTE ya China Bwana Huang Dabin ofisini kwake Ikulu leo Dk.
Shein amesema mradi wa ujenzi wa mindombinu ya Mfumo wa Mawasiliano ya
Habari na Tekinolojia unaotekelezwa na Kampuni ya ZTE kutoka China
unalenga katika kutoa fursa kwa Serikali na wananchi wa Zanzibar
kufaidika na matumizi ya sayansi na tekinolojia.
Alieleza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo ambao unajulikana zaidi kwa jina la e-government ambao
unajumuisha uwekaji wa mkonga wa mawasiliano pamoja na kuunganisha
mkonga huo na miundombinu ya mfumo wa mawasiliano Zanzibar ni hatua
muhimu katika ya kuiweka Zanzibar katika ramani ya matumizi ya
tekinolojia hiyo, hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi na kuharakisha
maendeleo.
Dk. Shein aliishukuru kampuni ya
ZTE kwa kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huo ambao hivi sasa
unaingia katika awamu nyingine ambayo itajumuisha matumizi ya
tekinolojia hiyo katika sekta ya afya na kodi.
Alibainisha kuwa hiyo ni hatua
nzuri ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kuimarisha matumizi ya tekinolojia ya habari na mawasiliano katika
shughuli za Serikali ili kuongeza ufanisi katika utendaji na kuboresha
utoaji huduma kwa wananchi.
Kwa hivyo, alitoa wito kwa Kampuni
ya ZTE katika kutekeleza awamu ya pili ya mradi, kuweka mkakati wa
kuelimisha jamii juu ya matumizi ya tekinolojia ya habari na mawasiliano
kwa kuwa mwamko wa matumizi ya teknolojia hiyo miongoni mwa watumishi
na viongozi wa Serikali pamoja na wananchi bado si wa kuridhisha.
Aliongeza kuwa lengo la Serikali
ni kukamilisha awamu ya pili ya mradi huo ili kutoa fursa kwa mradi huo
kuendelea kwa awamu nyingine ambayo itazihusisha sekta za elimu na
utalii.
Mhe. Rais alimuhakikishia Bwana
Huang kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufanya kazi na
kampuni hiyo na ameikaribisha kuangalia maeneo mengine ambayo kampuni
hiyo ina utalaamu na uzoefu ambayo inaweza kushirikiana na Serikali kama
uvuvi, utalii na afya.
Wakati huo huo Makamu wa Rais
Mwandamizi wa Kampuni ya ZTE Bwana Huang Dabin ameeleza kuwa
ameridhishwa kuona kampuni yake imeweza kukamilisha awamu ya kwanza ya
mradi huu ambapo sasa mradi umeingia katika awamu ya pili.
Alibainisha kuwa katika awamu ya
pili, mradi unahusisha kuzifikishia Ofisi na taasisi za Serikali huduma
za mkonga wa mawasiliano na kuuwezesha mfumo wa kodi nchini kutumia
tekinolojia hiyo pamoja na kuiwezesha Wizara ya Afya kutumia tekinolojia
hiyo katika kutoa huduma kwa wagonjwa.
Alifafanua kuwa chini ya matumizi
ya mfumo huo wa mawasiliano katika sekta ya afya, kumbukumbu za mgonjwa
zitaweza kupatikana katika hospitali yoyote atakayokwenda mgonjwa bila
ya kulazimika kutembea na mafaili yake.
Bwana Huang alisisitiza kuwa azma
ya kampuni yake ni kuifanya Zanzibar iweze kutumia mfumo wa tekinolojia
ya habari na mawasiliano katika shughuli zote na kuifanya Zanzibar
ing’are katika matumizi ya tekinolojia hiyo.
Kwa hivyo alibainisha kuwa Kampuni
yake imekusudia kujenga vituo sita vya kijamii vya matumizi ya
teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo watoto na vijana watajifunza
na kuvitumia ili kuhamasisha
Post a Comment