
Hayo
yalisemwa jana na Mkurugenzi Taasisi ya sekta binafsi(TPSF), Gideon
Kaunda katika mkutano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP)
katika uzinduzi wa kanuni za utawala bora katika biashara.
Alisema
suala la rushwa halipo upande mmoja ni muhimu kuhakikisha
wafanyabiashara wanaepuka rushwa kwani wafanyabiashara wote sio safi
hivyo ni lazima hatua zichukuliwe kwa wafanyabiashara wote.
Alisema
kanuni hizo zitasaidia kuleta maendeleo ya uchumi kwani UNDP wataleta
misaada ambayo itasaidia kueneza utawala bora na kuhamasisha watu katika
mikoa yote kuepuka rushwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Daniel Machemba alisema
uzinduzi huo ni juhudi za umoja wa mataifa kwa wafanyabiashara katika
kuondoa rushwa kwenye biashara.
“Wafanyabiashara wengi wamekuwa
wakipenda utajiri wa haraka na kuleta biashara ambazo hazina ubora ili
wao wafanikiwe kwa haraka,” alisema Machemba.
Naye Mshauri mwandamizi
wa Utawala, Steve Lee alisema uzinduzi huo ni muhimu kwani utawasaidia
wafanyabiashara kuelewa maadili na kuepukana na masuala yote ambayo
yanaweza kusababisha rushwa katika biashara.
Post a Comment