VIFO VIMENITOA FUNGATE - VANITHA

MSANII Vanitha Omary aliyeolewa hivi karibuni, amesema vifo vya mfululizo vya wasanii wenzake vimemlazimu kuondoka katika fungate ili ashirikiane na wenzake katika shughuli za misiba.
 

Vanitha aliyefunga ndoa siku moja kabla ya kifo cha msanii Recho Haule, alisema marehemu huyo alikuwa ni mtu wake wa karibu hivyo akalazimika kufuta mapumziko hayo ya baada ya ndoa.
“Tangu niolewe balaa juu ya balaa, hata sijafaidi ndoa yangu katika fungate, maana ilipita siku moja tu nikapata msiba wa Recho, tukamaliza ili tupumue, ukaja wa George Tyson ambaye naye alikuwa ananihusu sana, nikalazimika kuonyesha ushirikiano,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post