Mwito huo ameutoa juzi mjini hapa alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa chama cha waandishi wa
habari mkoa wa Mtwara (MTPC).
Alisema kwa kufanya hivyo atakuwa anatetea demokrasia ambayo inatoa haki kwa wote kusikilizwa na kufanya mikutano ya hadhara.
“Tunaomba
Msajili wa Vyama vya Siasa aachane na mambo ya ndani ya chama chetu kwa
sasa yeye analo jukumu kubwa la kuongea na mamlaka za juu za serikali
ili amri ya kupiga marufuku kwa mikutano ya hadhara iondolewe hivyo nasi
tupate haki ya kufanya mikutano na kuongea na wanachama wetu", alisema
Bingwe.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wao kama chama mara kadhaa
wameiomba serikali kuondoa amri hiyo kwani sasa hali ya amani imerejea
katika mikoa hiyo lakini bado haijatekeleza ombi hilo hivyo ni nafasi ya
msajili kuitumia nafasi hiyo kwani anawajibika pia kuona vyama
vikifanya mikutano katika maeneo yote ya nchi kama ilivyo sheria
anayoisimamia.
Mikoa ya Lindi na Mtwara iliwekewa marufuku ya
kutofanya mikutano ya hadhara ya kisiasa na mingineyo kwa muda
usiojulikana kutokana na vurugu zilizojitokeza mwanzoni mwa mwaka jana
zilizosababishwa na kundi la baadhi ya wakazi wa mikoa hiyo kupinga
mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara kuja
Dar es Salaam.
Post a Comment