FIFA:- Wachezaji wote ni waadilifu katika kombe la Dunia 2014(Video)

Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa traarifa za kufurahisha baada ya kuwafanyia vipimo wachezaji wote waliokwenda nchini Brazil, sambamba na timu zao za taifa kwa ajili ya kushiriki fainali za kombe la dunia.
FIFA limetoa taarifa hizo usiku wa kuamkia hii leo kupitia kwa mkuu wa kitengo cha tiba za wachezaji, Jiri Dvorak baada ya kuwafanyia vipimo wachezaji 736 waliofika nchini humo.
Jiri Dvorak, amesema wachezaji walikuwa wakipimwa mara kwa mara kabla na baada ya michezo waliyokuwa wakicheza, lakini majibu yaliyopatikana hakuna hata mchezo mmoja ambaye alikutwa na chembe chembe za dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Mkuu huyo wa kitengo cha tiba ameongeza kuwa mfumo wa kuwafanyia vipimo wachezaji wote haujaanza kuchukua nafasi yake kwenye fainali za mwaka huu, bali walianza tangu mwaka 2011 kwenye michuano ya klabu bingwa duniani ambayo ilifanyika nchini Japan na kisha waliendelea katika michuano mingine iliyo chini ya FIFA.


Wapo wachezaji ambao walidhaniwa huenda walitumia dawa hizo, kama mlinda mlango wa timu ya taifa ya Marekani, Tim Howard kufutia uwazo mkubwa aliouonyesha wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ubelgiji, pia mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Costa Rica, Brian Luiz naye aliwekewa mashaka kutokana na uhodari mkubwa alioudhihirisha wakati wa mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Italia.
Hata hivyo FIFA imesisitiza kuendelea kufanya vipimo kwa wachezaji wa timu zilizosalia kwenye fainali za kombe la dunia mpaka hapo kipyenga cha mwisho kitakapo pulizwa July 13.

Post a Comment

Previous Post Next Post