Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa traarifa za
kufurahisha baada ya kuwafanyia vipimo wachezaji wote waliokwenda nchini
Brazil, sambamba na timu zao za taifa kwa ajili ya kushiriki fainali za
kombe la dunia.
FIFA limetoa taarifa hizo usiku wa kuamkia hii leo kupitia kwa mkuu
wa kitengo cha tiba za wachezaji, Jiri Dvorak baada ya kuwafanyia vipimo
wachezaji 736 waliofika nchini humo.
Jiri Dvorak, amesema wachezaji walikuwa wakipimwa mara kwa mara kabla
na baada ya michezo waliyokuwa wakicheza, lakini majibu yaliyopatikana
hakuna hata mchezo mmoja ambaye alikutwa na chembe chembe za dawa za
kuongeza nguvu michezoni.
Mkuu huyo wa kitengo cha tiba ameongeza kuwa mfumo wa kuwafanyia
vipimo wachezaji wote haujaanza kuchukua nafasi yake kwenye fainali za
mwaka huu, bali walianza tangu mwaka 2011 kwenye michuano ya klabu
bingwa duniani ambayo ilifanyika nchini Japan na kisha waliendelea
katika michuano mingine iliyo chini ya FIFA.
Wapo wachezaji ambao walidhaniwa huenda walitumia dawa hizo, kama
mlinda mlango wa timu ya taifa ya Marekani, Tim Howard kufutia uwazo
mkubwa aliouonyesha wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya
Ubelgiji, pia mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Costa Rica,
Brian Luiz naye aliwekewa mashaka kutokana na uhodari mkubwa
alioudhihirisha wakati wa mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Italia.
Hata hivyo FIFA imesisitiza kuendelea kufanya vipimo kwa wachezaji wa
timu zilizosalia kwenye fainali za kombe la dunia mpaka hapo kipyenga
cha mwisho kitakapo pulizwa July 13.
إرسال تعليق