Wezi wa vyuma chakavu nchini Afrika kusini wameiba takribani kilomita 10 za reli ya mizigo inayotumika na kusababisha uharibifu wa takribani dola milioni 2.3.
Kipande cha reli hiyo kilichoharibiwa vibaya kimesababishwa na wezi
waliotekeleza uhalifu huo miezi kadhaa iliyopita kutoka sehemu
inayosafirisha treni kutoka mji wa Johannesburg hadi Nigel, ambapo
wanaume watano wamefikishwa mahakamani baada ya kukutwa wakifanya
kitendo hicho na askari waliokuwa doria.
Mmoja wa viongozi wa kamati ya usafirishaji ya Afrika Kusini Thumbu
Mahlangu,amenukuliwa akisema kuwa wezi hao ni wataalamu sana na
hawafanyi makosa wanapofanya uhalifu wao.
Tatizo la wizi wa vyuma kwenye reli limekuwa likikumba nchi nyingi za
kiafrika ikiwemo Tanzania ambapo wahalifu wamekuwa wakiharibu
miundombinu ya reli na wakati mwingine kusababisha ajali kutokana na
wizi huo.
إرسال تعليق