HIVI NDIVYO TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI ILIVYOPATA MAPOKEZI YA NGUVU NYUMBANI

Maelfu ya mashabiki wa soka nchini Ujerumani wamejitokeza mjini Berlin kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa walioshinda Kombe la Dunia.
Sherehe kubwa zimefanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambapo wachezaji wameonesha kombe waliloshinda kwenye jukwaa, huku wakiserebuka.
Watu wengi walikusanyika tangu alfajiri kuwakaribisha wachezaji hao waliowasili Jumanne asubuhi. Maelfu ya watu pia walijipanga pembezoni mwa barabara.
Hili ni kombe la nne la dunia kwa Ujermani kushinda, na la kwanza kwa Ujerumani iliyoungana tena mwaka 1990.

Post a Comment

أحدث أقدم