Carlos
Queiroz alijiuzulu nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya Iran baada
ya nchi hiyo kutolewa hatua ya makundi katika fainali za kombe la dunia
mwaka huu nchini Brazil.
HAPA tunaangalia kwanini Asia imeshindwa kufanya vizuri katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
1. UKOSEFU WA UONGOZI
Wakati
kocha wa Korea Hong Myung-bo anasafiri kwenda Uholanzi mwezi machi mwaka
huu kumtembelea Park Ji-sung, hakwenda kuangalia wachezaji muhimu bali
ni kumshawishi nyota huyo aachane na mpango wa kustaafu soka la
kimataifa.
“Timu ya
vijana inahitaji wakongwe,” alisema Hong. Park alipotezea wazo lile,
lakini ni ukweli kuwa Korea ilikosa wachezaji wenye uzoefu na viongozi
kama yeye. Pia Japan haikuwa na wachezaji ambao wangepewa majukumu ya
kuwaongoza vijana uwanjani katika mazingira tofauti tofauti ya mechi.
2. MAKOSA YA MAKOCHA
Alberto
Zaccheroni alikuwa na maandalizi kamili yaliyochukua hadi miaka minne
tangu alipokabidhiwa timu ya Japan, lakini bado kocha huyo raia wa
Italia hajaweza kuonesha kiwango kizuri katika hatua ya makundi. Japan
ilicheza mpira wa kawaida dhidi ya Ivory Coast na Ugiriki.
Alikosolewa
kwa kumuanzisha Yasuhito Endo dhidi ya Waafrika, pia aliendelea
kumuacha Yasuyuki Konno katika idara ya ulinzi wakati alishindwa kufanya
kazi yake na angemtumia hata Zaccheroni kutokana na kiwango chake kuwa
kizuri kwa wakati ule.
Kocha wa
Korea, Hongg, hakuwa na wachezaji wenye uzoefu, lakini alishindwa
kuwatumia vijana wake katika safu ya ulinzi na hakusikiliza ushauri wa
vyombo vya habari na mashabiki na kuendelea kumtumia mshambuliaji butu
Park Chu-young. Carlos Queiroz alikuwa na kiwango kizuri, labda atajuta
baada ya kushindwa kuonesha ubora wake na kuisaidia timu kwenye mechi
dhidi ya Bosnia.
3. NYOTA HAWAKUNG`ARA
Keisuke
Honda, Shinji Kagawa, Park Chu-young, Shinji Okazaki na Lee Chung-yong
ni baadhi ya wachezaji wakubwa ambao hawakufanya lolote. Wengine
wanaweza kusingizia hali ya klabu zao kwa kusababisha kushuka kiwango,
lakini sio sababu kubwa.
Honda
angalau alianza vizuri dhidi ya Ivory Coast, lakini Kagawa hakufanya
lolote. Watu wengi wa Korea walipinga mawazo ya Park kuichezea nchi yake
wakati hajawahi kucheza katika klabu yake na kwakweli walikuwa sahihi.
Kama wachezaji wazuri hawako katika kiwango chao, hapo lazima timu
yoyote iwe na matatizo.
4. KUKOSA MORALI YA USHINDI
Kuna
maandishi mengi yameandikwa kuonesha jinsi gani hamu ya kushinda
inavyosaidia mataifa madogo kama Uruguay kufanya vizuri katika michuano
mikubwa. Baadhi ya timu za Asia zinatakiwa kujifunza jambo hili. Baadhi
ya timu na wachezaji wake wanajitahidi kucheza kadiri wawezavyo ili
kuibuka na ushindi. Kwa timu kama Japan na Korea kusini, wanatakiwa
kulifikiria hili. Kucheza mpira wako ni vizuri, lakini wakati mwingine,
unatakiwa kuangalia namna ya kupata ushindi, lazima uwe na hamu na
kutumia mbinu nyingi zaidi.
5. KUKOSA BAHATI
Wakati
mwingine unaweza kuamini. Iran wangepata penati kwenye mechi dhidi ya
Argentina, wangeondoa gundu ya Asia ya kutopata ushindi.
Pia
wachezaji waliotea wakati Urusi wanasawazisha goli dhidi ya Korea kusini
na kama maamuzi yangekuwa sahihi mambo yangekuwa tofauti ambapo
wangepata pointi tatu za kwanza. Kukosa bahati kuliwaathiri sana na
kufika pale walipofika.
Tim Cahill alionesha kiwango kizuri akiwa na Australia, lakini haikuwa na maana kwasababu walipoteza mechi zote za makundi.
6. ASIA INAYOENDELEA
Asia
ilianza kuendelea milongo mingi baada ya Ulaya na imeweza kufika mbali.
Ingawa Korea walifanya vibaya katika hatua ya kufuzu wakiwa na
shirikisho imara, walijitahidi na kufanikiwa. Japan nayo haikuwa nzuri
sana, lakini shirikisho lao bora liliwafanya waweze kufuzu.
Michuano
pekee ambayo inazikutanisha nchi za Asia na nje ya Asia inakuja kila
baada ya miaka minne, hii inapelekea timu hizo kwenda kombe la dunia
zikiwa hazina ubora wa kutosha. Asia ipo katika wakati wa mpito katika
soka tofauti na Ulaya pamoja na Amerika. Nchi nyingi zinajikongoja na
ndio maana zinashindwa kufanya makubwa.
7. MAKIPA HAWAKUWA KWENYE VIWANGO BORA
Kumekuwepo na makipa bora kutoka Asia miaka ya karibuni, lakini kwa mashindano ya mwaka huu, makipa wengi hawakuwa wazuri.
Kipa wa
Iran, Alireza Haghighi, peke yake ndiye alikuwa kipa aliyeonesha kiwango
cha juu katika fainali za Brazil. Wengine hawakufanya vizuri. Kipa wa
Australia. Mat Ryan alionesha kiwango kizuri, lakini angefanya vizuri
zaidi hususani kwenye mechi dhidi ya Uholanzi.
Kipa wa
Japan, Eiji Kawashima alikuwa tatizo na alifanya makosa makubwa kwenye
mechi dhidi ya Ivory Coast. Jung Sung-ryeong wa Korea kusini hakuonesha
kiwango kizuri dhidi ya Urusi na Algeria.
8. KUKOSEKANA KWA WASHAMBULIAJI BORA
Ni swali
la kizamani kidogo. Kitendo cha timu nyingi za bara hilo kuwa na
washambuliaji wengi wa kigeni ni kwasababu hakuna washambuliaji wa
nyumbani au hakuna wachezaji wazawa wa kutosha?, bila kujali sababu,
kukosekana kwa wafungaji katika bara hilo limekuwa tatizo kwao hasa
katika fainali za kombe la dunia. Wote Yuya Osako, Yoichiro Kakitani,
Park Chu-young au Kim Shin-wook hawakufunga. Tim Cahill, ambaye amekuwa
akicheza kama kiungo katika klabu yake, ni mshambuliaji pekee ambaye AFC
walikuwa naye Brazil.
9. MAKUNDI MAGUMU
Pengine
kwa upande wa Austaralia walijitahidi kwenye kundi lao lililokuwa na
nchi za Uholanzi, Chile na Hispania. Nchi za Asia zilipangwa katika
makundi magumu. Makundi ya Korea na Japan pengine yalikwa magumu zaidi.
Korea walikuwa na nchi za Ubelgiji, Algeria na Urusi. Japan wao
walikuwa na Bosnia, Argentina, na Nigeria
10. SIASA
Iran wana
mapenzi ya soka na vipaji pia vipo. Kidogo mambo yalikwenda tofauti,
lakini wangewashinda Argentina, labda wangeenda raundi ya pili. Nchi hii
ingekuwa timu nzuri kama hali ya kisiasa ingekuwa shwari .Kumekuwa na
athari kubwa ya siasa katika shirikisho la Iran. Kama kungekuwa na
utulivu, serikali ingetoa sapoti kubwa kwa shirikisho na pengine mambo
yangekuwa mazuri.
إرسال تعليق