Msanii Ommy Dimpoz aka Poz Kwa Poz alikuwa ni mmoja wa wasanii walioweza kutamka katika mtandao wankijamii Twitter kuwa “Huu ni Ubaguzi” na vile vile bila kusahau malalamiko haya hajaanza leo wala jana na sio kwamba hawa ni wasanii wa wanza kupewa awards kabla ya muda wa show ya A LIST.
“Hata muda wa kilele cha utoaji tuzo haujafika lakini Kipengele cha wawakilishi wa Africa washatangaza mshindi na kashapewa tuzo #Ubaguzi” OMMY DIMPOZ
“Nashindwa kuelewa kwani Hawa BET hawa wawakilishi wetu wa Africa wakiwapa tuzo muda mmoja na wasanii wa Marekani watapungukiwa nini #Ubaguzi” OMMY DIMPOZ
Baada ya kufanya utafiti wa huku na kule kutaka kujua nini hasa kinachosababisha hivyo nimegundua kuwa kila mtu ana mipango yake katika swala kama hili au mipango yao wanavyoamua, navyoona mimi ni bora kushukuru kwa kishirikishwa kwenye kitu kama hicho ambacho kinasaidia Publicity ya kutosha kwa hata kutamkwantu jina la msanii na nchi aliyotoka na kwa kiwango cha muziki tulichonacho haswa kwa nchi kama Tanzania sababu hata wao hatujawahi kusikia wakilalamika hawajashirikishwa na kupewa Awards kwenye TUZO za KTMA. Cha muhimu ni kujishughulisha na kwetu na kushukuru hicho kiasi kidogo ambacho wameamua wao kutoka kwenye “TUZO ZAO”….. Na jamani tuelewe kuwa hizo tuzo ni za kwao wao na maamuzi ni ya kwao, kama wanavyoamuaga ‘KTMA’ kuwapa TUZO wasanii wasiostahiri na wengi wetu tunajuaga na kulalamika kwenye vyombo vya habari na tunaacha yanapita kwa hiyo ulalamishi sio mzuri sababu hautufikishi popote na hautasaidia chochote, na maneno mengine kama “UBAGUZI” sio mazuri sababu wenzetu wale wa Marekani wausi wamebaguliwa kweli sio kwa maneno na kwa kiasi kikubwa neno kama hilo wanachukulia “personal” sana. Nachoona muhimu ni kuhangaika na vyetu “Kivyetuvyetu” kupigania cha kwetu kwanza (KTMA) kuweka sawa na kusimamia hizi tuzo zetu kwanza zisiwe na urasimu unaoendela mpaka leo kuliko kuzungumzia nankushutumu TUZO za BET ambazo zilianzishwa kwa ajili ya ‘African American’ ambao walinyanyaswa na kuwekwa kando kwenye Tuzo nyingine za nchini humo kwa miaka mingi sana.
Kuna comment ambayo nimeikuta Online kutoka kwa bwana ‘Chris Vincent’s’ Kutoka nchini ‘Ghana’ ambayo naona ni nzuri pia hata BET wakiiona inaweza kuwafanya wabadilishe mipango yao na kutufikiria kutuweka stage moja na wao…. Comment hiyo ambayo iliandikwa mwaka Jana kwamba….
“A single category for a whole continent must be given priority… If BET cannot find 5 mins for the whole BIG AFRICA on stage, then they should not invite us NEXT TIME! We have other important things to do down here… Even if nothing at all, we got monkeys to chase and climb trees with!”
إرسال تعليق