Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Isaya Mngulu
akishauriana na maafisa wake leo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014
majira ya saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini
Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa,
Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi
huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni:
1. SHAABAN MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26 Kabila,
Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
2. ATHUMAN HUSSEIN
MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo
eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
3. MOHAMED NURU @
MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani
na eneo la tukio.
4. JAFFAR HASHIM
LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya
Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha. Huyu ametambuliwa
kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo
mbalimbali nchini.
5. ABDUL MOHAMED
HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
6. SAIDI MICHAEL
TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU
HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA ,
kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa
walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun, mapanga
mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja.
Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa
ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya
milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi
mwa Polisi na kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa
matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA
HASSAN HELLA, kabila mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye
asili ya eneo la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya
ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa
zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano
mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
………………...…………..
ISAYA MNGULU-CP
MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA
إرسال تعليق