TRA KUTOA TIN, STIKA ZA MAGARI SABASABA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kutoa huduma za namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) kwa watu binafsi, na stika za ada ya magari kwa mwaka katika maonesho ya Sabasaba.

Aidha, imewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti kwa kutumia mashine za kielektroniki za utoaji wa risiti (EFDs) kwa wale waliosajiliwa na wanatakiwa kutoa risiti hizo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, jana  katika  Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, maarufu kama Sabasaba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Aliwataka wananchi kujitokeza kupata TIN namba zao ambazo siyo za kibiashara,  kwani zile za biashara zina mlolongo mrefu unaotaka mahesabu.

“Pia tutatoa maelezo ili kutoa ujumbe wa wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kupokea klabu za shule za wanafunzi wa sekondari kwa ajili ya kujenga uzalendo,” alisema Kayombo.

Akizungumzia suala la utaoji wa risiti za EFDs, alisema washiriki wakiuza bidhaa watoe risiti kwa kuwa maofisa wa mamlaka hiyo, watakuwa wanapita kukagua kuona kama agizo hilo linatekelezeka.

Post a Comment

Previous Post Next Post