Aidha, imewataka
wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti kwa kutumia mashine za
kielektroniki za utoaji wa risiti (EFDs) kwa wale waliosajiliwa na
wanatakiwa kutoa risiti hizo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Idara
ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, jana katika
Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, maarufu kama Sabasaba katika
Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Aliwataka
wananchi kujitokeza kupata TIN namba zao ambazo siyo za kibiashara,
kwani zile za biashara zina mlolongo mrefu unaotaka mahesabu.
“Pia
tutatoa maelezo ili kutoa ujumbe wa wananchi kujenga tabia ya kulipa
kodi ikiwa ni pamoja na kupokea klabu za shule za wanafunzi wa sekondari
kwa ajili ya kujenga uzalendo,” alisema Kayombo.
Akizungumzia suala
la utaoji wa risiti za EFDs, alisema washiriki wakiuza bidhaa watoe
risiti kwa kuwa maofisa wa mamlaka hiyo, watakuwa wanapita kukagua kuona
kama agizo hilo linatekelezeka.
إرسال تعليق