Wafuasi wa CCM,CHADEMA nusura wazitwange mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla

01
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi wetu
Jitihada za Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuwazuia wananchi wasiendelee kumzomea Naibu waziri wa maji Amos Mkala jana zilimuokoa Waziri huyo na kuweza kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu ya upatikanaji wa maji katika jimbo la Ubungo.
Kabla ya makala kuanza kuzomewa wananchi waliokuwa na bendera za Chama cha Mapinduzi,waliuteka  kwa muda ziara hiyo ya Kiserikali huku viongozi wao wakiugeuza kuwa wa kichama zaidi na kuanza kumzomea Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyekuwa katika ziara hiyo
Wakiwa na mabango ya kulaani kukosekana kwa maji wanachama hao wa CCM pasipo kujali kama serikali iliyo madarakani ndiyo kikwazo cha hali hiyo walimlaumu Mnyika kuwa hawasaidii na kuamua kumzomea kila alipokuwa akiongea hali iliyofurahiwa na Amos Makala.
Hata hivyo Mnyika aliweza kuzishinda hisia hizo na kutoa ufafanuzi wa namna anavyowapigania wakazi wa Kimara Mavurunza na maeneo mbali mbali ya jiji kupata maji pasipo kujali itikadi zao za kivyama.
Akiongea huku akiwa ni mwenye kutabasamu Mnyika alisema ziara hiyo ya Naibu waziri ni matokeo yake ya kumbana waziri wa maji PROFESA Jumanne Maghembe, pamoja na watendaji wa Dawasa kuhakikisha maji yanapatikana kwa wakazi wa Dar esSalaam,
Alisema  kushindwa kwa serikali ya CCM, kuzuia wizi wa maji unaofanywa na watu wanaouza maji, hususan viongozi wa serikali, tatizo la maji linsingekuwa kwa kiasi kinachotisha kama ilivyo sasa.
Alimtaka naibu Waziri Makala ahakikishe wakazi wa Ubungo na maeneo mengine ya jiji wanapata maji kwa kuwa ni haki yao ya msingi na kwamba wawabane watu wanaouza maji.
02
Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika  akihutubia na Wana Chadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla  akihutubia katika mkutano huo.
Baada ya Mnyika kumaliza kuzungumza alisimama Amos Makala na kabla hajaanza kuongea wananchi walimueleza kuwa hawataki porojo zaidi ya maji
“Kiongozi hapa tunataka maji hizo porojo zako za kisiasa peleka huko huko kwa kuwa tumechoka na ahadi zisizotekelezeka kwa muda wa miaka hamsini”alisema Mwananchi ambaye hakufahamika jina
Makala badala ya kutulia alimueleza mwananchi huyo kama hataki porojo aondoke katika mkutano hali ilizua zomea zomea kutoka kwa wananchi.
Baada ya hali hiyo akiwa amekasirika Makala aliwatishia kuwakamata kwa kuwaita polisi,hata hivyo  zoezi hilo lililoshindikana kutoka na uchache wa polisi waliokuwepo.
Katika jitihada zake za kuendelea kuwatisha wananchi Makala alitaka kuwafuata huku, Mnyika akimzuia na kumueleza hali hiyo isingekuwepo kama wasingeingiza siasa katika masuala ya kiserikali
 Hata hivyo Mnyika aliwasihi wananchi wampe nafasi kiongozi huyo aweze kuwaeleza mipango ya Serikali.
Baada ya Ombi hilo la Mnyika wananchi walitulia na Makala akaeleza kuwa serikali imeshatenga kiasi cha sh bilioni 362 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Ruvu juu na chini na kwamba miradi hiyo itakamilika ifikapo septemba mwakani
Pia makala alisema katika kuboresha maeneo ya kutunzia maji matanki ya Kimara yatavunjwa na kujengwa upya kwa ajili ya kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji zaidi.
03
Polisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
04
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru polisikuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM juu ya maji, huku Mnyika akitaka waendelee kuzomea akidai kwamba Waziri hakufanya haki kwani yeye alipokuwa akizomewa na Wana CCM hakuwachukulia hatua kama hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya Mavurunza, kata ya Salanga
Mfuasi wa CCM  akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
07
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, Eva Sinare (katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema.
IMG_0196
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo.
IMG_0232
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara.
IMG_0243
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa  jiji la Dar es Salaam kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi wake umeanza sasa.
IMG_0281
Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.
IMG_0310
Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swali katika mkutano uliofanyika Kata ya Kibamba.
IMG_0311
Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo.
Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
IMG_0344
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam, (Dawasco), Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa maji katika kata hiyo.
IMG_0354
Wafuasi wa CCM  na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwa kwenye magari eneo la Kibamba. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG).

Post a Comment

Previous Post Next Post