Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa
Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa
CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea
mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo,
Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi wetu
Jitihada
za Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuwazuia wananchi wasiendelee kumzomea
Naibu waziri wa maji Amos Mkala jana zilimuokoa Waziri huyo na kuweza
kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu ya upatikanaji wa maji
katika jimbo la Ubungo.
Kabla
ya makala kuanza kuzomewa wananchi waliokuwa na bendera za Chama cha
Mapinduzi,waliuteka kwa muda ziara hiyo ya Kiserikali huku viongozi wao
wakiugeuza kuwa wa kichama zaidi na kuanza kumzomea Mbunge wa Ubungo
John Mnyika aliyekuwa katika ziara hiyo
Wakiwa
na mabango ya kulaani kukosekana kwa maji wanachama hao wa CCM pasipo
kujali kama serikali iliyo madarakani ndiyo kikwazo cha hali hiyo
walimlaumu Mnyika kuwa hawasaidii na kuamua kumzomea kila alipokuwa
akiongea hali iliyofurahiwa na Amos Makala.
Hata
hivyo Mnyika aliweza kuzishinda hisia hizo na kutoa ufafanuzi wa namna
anavyowapigania wakazi wa Kimara Mavurunza na maeneo mbali mbali ya jiji
kupata maji pasipo kujali itikadi zao za kivyama.
Akiongea
huku akiwa ni mwenye kutabasamu Mnyika alisema ziara hiyo ya Naibu
waziri ni matokeo yake ya kumbana waziri wa maji PROFESA Jumanne
Maghembe, pamoja na watendaji wa Dawasa kuhakikisha maji yanapatikana
kwa wakazi wa Dar esSalaam,
Alisema
kushindwa kwa serikali ya CCM, kuzuia wizi wa maji unaofanywa na watu
wanaouza maji, hususan viongozi wa serikali, tatizo la maji linsingekuwa
kwa kiasi kinachotisha kama ilivyo sasa.
Alimtaka
naibu Waziri Makala ahakikishe wakazi wa Ubungo na maeneo mengine ya
jiji wanapata maji kwa kuwa ni haki yao ya msingi na kwamba wawabane
watu wanaouza maji.
Wafuasi
wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo
ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika akihutubia na Wana Chadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla akihutubia katika mkutano huo.
Baada
ya Mnyika kumaliza kuzungumza alisimama Amos Makala na kabla hajaanza
kuongea wananchi walimueleza kuwa hawataki porojo zaidi ya maji
“Kiongozi
hapa tunataka maji hizo porojo zako za kisiasa peleka huko huko kwa
kuwa tumechoka na ahadi zisizotekelezeka kwa muda wa miaka
hamsini”alisema Mwananchi ambaye hakufahamika jina
Makala
badala ya kutulia alimueleza mwananchi huyo kama hataki porojo aondoke
katika mkutano hali ilizua zomea zomea kutoka kwa wananchi.
Baada
ya hali hiyo akiwa amekasirika Makala aliwatishia kuwakamata kwa
kuwaita polisi,hata hivyo zoezi hilo lililoshindikana kutoka na uchache
wa polisi waliokuwepo.
Katika
jitihada zake za kuendelea kuwatisha wananchi Makala alitaka kuwafuata
huku, Mnyika akimzuia na kumueleza hali hiyo isingekuwepo kama
wasingeingiza siasa katika masuala ya kiserikali
Hata hivyo Mnyika aliwasihi wananchi wampe nafasi kiongozi huyo aweze kuwaeleza mipango ya Serikali.
Baada
ya Ombi hilo la Mnyika wananchi walitulia na Makala akaeleza kuwa
serikali imeshatenga kiasi cha sh bilioni 362 kwa ajili ya kuboresha
miundombinu ya Ruvu juu na chini na kwamba miradi hiyo itakamilika
ifikapo septemba mwakani
Pia
makala alisema katika kuboresha maeneo ya kutunzia maji matanki ya
Kimara yatavunjwa na kujengwa upya kwa ajili ya kuwa na uwezo wa
kuhifadhi maji zaidi.
Polisi
wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John
Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo
aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge
kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,
John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru
polisikuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza
Utakelezaji wa Ilani ya CCM juu ya maji, huku Mnyika akitaka waendelee
kuzomea akidai kwamba Waziri hakufanya haki kwani yeye alipokuwa
akizomewa na Wana CCM hakuwachukulia hatua kama hiyo katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya Mavurunza, kata ya Salanga
Mfuasi wa CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, Eva Sinare
(katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri
wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo.
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani
ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa jiji la Dar es Salaam
kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia
hasa baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao
ujenzi wake umeanza sasa.
Makalla
akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la
maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua
miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.
Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swali katika mkutano uliofanyika Kata ya Kibamba.
Mwalimu
wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa
waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo.
Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam, (Dawasco),
Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata
ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa
maji katika kata hiyo.
Wafuasi
wa CCM na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao
wakiwa kwenye magari eneo la Kibamba. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO
BLOG).
إرسال تعليق