Lady Jaydee: Hata ndoa yangu ikivunjika haimaanishi mnitafutie story za kunichafua, ajibu kwa urefu habari iliyoandikwa na gazeti la udaku

Lady Jay Dee, jana (August 30) kupitia Instagram alijibu kwa ufupi habari iliyoandikwa na gazeti la Risasi yenye kichwa cha habari ‘Jide, dogo dogo gumzo mjini’, (Ingia hapa).Leo kupitia ukurasa wake wa Facebook amejibu kwa urefu zaidi juu ya habari hiyo.
jide
Hivi ndivyo alivyoandika Jide:
Zamani ilikuwa haipo sehemu ya kujitetea, gazeti likishaandika ndio limeandika.
Lakini sasa ulimwengu umebadilika, sio muda wa watu wote kulishwa chakula kisichofaa.
Kwanza hicho kichwa cha habari kimenivunjia heshma sana

Nafikiri lengo ni kuilazimisha jamii inayomuelewa JayDee tofauti imuone kuwa ni mtu asiefaa, sawa.

Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni mimi nilizi post mwezi February Instagram?????
Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge tena kutumia simu ya Gardner.
Jide, dogodogo gumzo mjini
Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na kilichoenea kila kona ,,,,,sasa hii habari ni gumzo wapi ambapo haisikiki, ……

Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide gumzo hili, ndio ningewaelewa.
Vitu vya kuzua.
Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi wanaomba kupiga picha na mimi na wengine pia wanaomba kupiga picha na gari sababu wanaipenda.

Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha na sanamu la kitu chochote anachokipenda.


SOMA STORY MZIMA KWAKUBOFYA HAPA.

Post a Comment

Previous Post Next Post