RACHAEL CLAVERY ASHINDA TAJI LA MISS LAKE ZONE 2014 JIJINI MWANZA,AJINYAKULIA GARI LA MIL 10

Mshindi wa Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya ( kushoto). 

Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza usiku huu. Shindano hilo lilikuwa na Walimbwende 18 wote wakichuana vikali na kila mmoja akitaka ashinde kabla ya Rachael Clavery kuwafunika wenzake na kuibuka na ushindi. 
Gari aliloshinda Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery usiku huu.
Warembo wote 18 jukwaani
Vazi la ufunguzi..warembo wote 18 walipanda jukwaani
Warembo waliopanda jukwaani ni Mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban: Doreen Robert; Christina Jilulu (Mwanza): Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na Rachael Julika (Shinyanga).
Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba: Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu). Wamo pia Martina John: Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara)huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita.

Post a Comment

Previous Post Next Post